Mtalaa wa shahada ya kwanza ya sanaa katika Kiswahili na mawasiliano katika chuo Kikuu cha Egerton unahusu vipengele viwili vinavyohusiana na kukamilishana; yaani lugha na mawasiliano. Jambo hili linalenga kuwatayarisha wanafunzi kupata ujuzi na maarifa yanayowezesha kuhudumu katika nyanja mbalimbali zinazohusu lugha na mawasiliano. Kwa njia hii, mtaala huu unaafikiana na lengo la chuo Kikuu cha Egerton la kuzalisha wasomi wenye ukakamavu na umahiri katika sekta mbalimbali. Mtalaa huu unawalenga wasomi wanaotarajia kuhudumu katika nyanja kama vile habari na utangazaji, ualimu wa lugha, uhariri, uchapishaji, huduma za jamii, tafsiri na fasiri, utafiti n.k.
Mitalaa ya lugha iliyopo kufikia sasa imekuwa ikitilia mkazo lugha bila kuihusisha na mawasiliano. Maendeleo katika nyanja ya teknolojia habari yamezua haja ya wataalam wa lugha wenye upeo mpana, na ambao wana uwezo wa kukabiliana na changamoto zinazowakumba katika utenda kazi wao. Aidha, ni muhimu lugha ifundishwe kwa kufungamanishwa na utumikizi wake katika nyanja mbalimbali za maisha.
Mwanafunzi wa B.A (Kiswahili na Mawasiliano) katika chuo kikuu cha Egerton ni mwanafunzi wa Kiswahili aliye na kipengele muhimu sana cha mawasiliano ambacho kitampa nafasi bora ya kuwahi kazi katika mashirika mbalimbali yanayoshrikisha mawasiliano katika nyanja mbalimbali kama vile vyombo vya habari, ualimu, mashirika yasiyo ya kiserikali, tafiti mbalimbali, kazi za mawasiliano mema na zile zinazohitaji tafsiri.
Mtalaa wa B.A (Kiswahili na Mawasiliano) unanuiwa kufundisha wataalam wenye ubunifu, ukakamavu, ujuzi na uwezo wa kujiunga na sekta mbalimbali za uchumi zinazojihusisha na lugha na mawasiliano, na kutoa mchango thabiti;
Mtalaa wa B.A (Kiswahili na Mawasiliano) unalenga kutoa fursa mahsusi kwa masomo ya kinadharia na masomo tumikizi. Inawatayarisha walengwa katika:
Mahitaji ya kawaida ya shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Egerton pamoja na yale ya kitivo cha elimujamii na maendeleo, yatatumika:
Zaidi ya kutimiza mahitaji haya, mwanafunzi atahitaji kuwa na alama ya C+ katika Kiswahili ili kujiunga na shahada ya B.A (Kiswahili na Mawasiliano).
Mtalaa wa BA (Kiswahili na mawasiliano) katika Chuo Kikuu cha Egerton utachukua muda wa miaka minne kwa wanafunzi wanaoshiriki kikamilifu. Wanafunzi wanaoshiriki kwa muda wataruhusiwa kuukamilisha mtalaa kwa kipindi cha miaka minane ;
Wanafunzi watafanya jumla ya CFs zisizopungua 18 katika kila muhula huku wakiwa na kozi sita; zote za lazima katika mwaka wa kwanza na wa pili. Katika mwaka wa tatu na wa nne wanafunzi watakuwa na kozi tano za lazima na kupewa fursa ya kuteua kozi moja ya hiari kila muhula ili kukamilisha matakwa ya kozi sita kila muhula;
Ili mwanafunzi wa kozi hii aweze kufuzu kikamilifu, atahitaji kuwa na CFs 149.5; 134 CFs zikiwa za Kiswahili na Mawasiliano na CFs 15.5 zikiwa baadhi za kozi za lazima zilizopendekezwa na chuo, kwa mwanafunzi yoyote yule.
Mahitaji ya kawaida ya shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Egerton pamoja na yale ya kitivo cha elimujamii na maendeleo, yatatumika:
Zaidi ya kutimiza mahitaji haya, mwanafunzi atahitaji kuwa na alama ya C+ katika Kiswahili ili kujiunga na shahada ya B.A (Kiswahili na Mawasiliano).